Jumbe muhimu
Afya ni haki ya binadamu; ni wakati wa kuwepo kwa mpango wa afya kwa wote.
Tunafahamu kuwa mpango wa huduma za afya kwa wote unawezekana, tujitahidi ili mpango huu ufaulu!
Mpango wa afya kwa wote unamaanisha kuwa watu wote wanaweza kupata huduma bora za afya wanazohitaji,kila wakati na mahali wanapozihitaji bila kusumbuka kifedha.
Nusu ya watu ulimwenguni huwa hawapokei huduma za afya wanazohitaji.
Takriban watu milioni 100 husukumwa katika umaskini mkubwa kila mwaka kwa sababu ya kugharimia huduma za afya kutoka mifukoni mwao.
Lakini je watu hawa ni akina nani na tunaweza kuwasaidia vipi? Ili kupata taswira kamili kuhusu ni nani ambaye hajajumuishwa, kulingana na maelezo kuhusu jinsia, umri, mapato, mahali na, elimu na sababu nyingine ambazo zinaathiri upatikanaji wa huduma za afya.
Afya ni haki ya binadamu; kila mmoja anastahili kuwa na habari na huduma anazohitaji ili kuitunza afya yake binafsi na afya ya familia yake.
Upataji wa huduma bora ya afya na ya kimsingi ndio dhamira ya mpango wa huduma za afya kwa wote.
Huduma duni za afya na zisizokuwa salama huangamiza maisha na kugharimu ulimwengu matrilioni ya dola kila mwaka, hivyo basi ni sharti tujizatiti zaidi kuimarisha ubora na usalama wa huduma za afya ulimwenguni.
Huduma ya kimsingi ya afya inastahili kuwa hatua ya kwanza ya kila mmoja kujumuishwa kwenye mfumo wa afya, ambapo watu binafsi, familia na jamii watatangulia kuenda ili kupokea huduma zao za afya-kuanzia hatua ya kuhimizwa, kupata kinga hadi kwa matibabu yenyewe, urekebishaji, na ufifishaji wa athari za magonjwa yasiyopona –huduma hizi zote wakizipata mahali karibu zaidi na wanakoishi na kufanya kazi.
Kuu katika dhamira yake, huduma ya afya za kimsingi, zinahusu hasa kuwatunza watu na kuwasaidia kudumisha afya yao nzuri badala ya kutibu tu ugonjwa fulani au hali moja maalum.
Huduma ya afya ya kimsingi hujumuisha mahitaji yako mengi ya kiafya maishani mwako; ambayo ni pamoja na huduma za kuchunguzwa kwa matatizo ya kiafya, chanjo, maelezo ya jinsi ya kuzuia maradhi, upangaji uzazi, matibabu ya maradhi yanayodumu kwa muda mrefu na yale yanayopona upesi, kushirikiana na ngazi nyingine za huduma za kimatibabu, na matibabu ya urekebishaji.
Huduma ya afya ya kimsingi ni njia yenye gharama nafuu na ya usawa ya kutoa huduma za afya na kusaidia mataifa kupiga hatua katika kutimiza mpango wa afya kwa wote.
Mfumo wa afya wenye huduma thabiti za afya ya kimsingi huchangia katika kuimarisha matokeo ya afya, huwa na gharama nafuu na huimarisha ubora wa huduma.
Wahudumu wa afya wana wajibu muhimu wakitakiwa kuelimisha wagonjwa kuhusu jinsi ya kuitunza afya yao, kushirikisha huduma za afya na kutetea, kwa mameneja wa hospitali na waundaji sera, mahitaji ya wagonjwa wao.
Wahudumu wa afya ya kimsingi wana uhusiano wa muda na wa kuaminika na wagonjwa wao na hujua historia yao ya kiafya; na kufahamu hali yao kamili husaidia kuimarisha tiba kwao na kuokoa pesa.
Wahudumu wa afya ya kimsingi wanafahamu mila, tamaduni na desturi za jamii wanazohudumu, na kuwafanya kuwa muhimu zaidi panapotokea mkurupuko wa magonjwa au hali ya dharura.
Ili kufanikisha mpango wa afya kwa wote, tunahitaji: watu binafsi na jamii waliowezeshwa kufikia huduma bora zaidi za afya ili waweze kutunza afya zao wenyewe na afya ya familia zao; wahudumu wa afya wenye ujuzi wanaotoa huduma bora zaidi na zinazoegemea kwa wanajamii; na waundaji sera waliojitolea kuwekeza katika huduma za afya za kimsingi.