Siku ya Afya Ulimwenguni mwaka wa 2019

Siku ya Afya Ulimwenguni mwaka wa 2019

Aprili 7

WHO/Yoshi Shimizu
© Credits

Mpango wa Afya kwa Wote

Mpango wa  Afya kwa wote ndiyo dhamira kuu ya WHO. Muhimu katika kufaulisha dhamira hii ni kuhakikisha kuwa kila mmoja anaweza kupata huduma za afya anapozihitaji na wakati anapozihitaji, pale katika jamii yake.

Hatua imepigwa katika mataifa katika kila pembe ya ulimwengu.

Lakini mamilioni ya watu bado hawawezi hata kidogo kupata huduma za afya. Mamilioni ya wengine hulazimika kuchagua kati ya huduma za afya na mahitaji mengine kama vile chakula, mavazi na hata makazi.

Hii ndiyo sababu WHO inazingatia kwa dhati  kuwepo kwa mpango wa afya kwa wote Siku hii ya Afya Ulimwenguni, mnamo Aprili 7.


Angaa nusu ya idadi ya watu ulimwenguni bado hawawezi kupata huduma muhimu za afya.

Hali ya mambo

Ni nini maana ya Mpango wa Afya kwa Wote?

Huduma ya afya ya kimsingi ni nini?